Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kufunga kabla ya Ramadhani kwa siku moja au siku mbili, kwa nia ya kuchukua tahadhari kuwa huenda Ramadhani imeingia; kwa sababu ulazima wa Ramadhani umewekwa katika kuonekana kwa mwandamo, na wala hakuna haja ya kujikalifisha, isipokuwa kama mtu alikuwa akifunga swaumu aliyoizoea, kama kufunga siku moja na kula siku moja, au siku ya juma tatu na Alhamisi ikaangukia siku hiyo basi na afunge; na wala hilo halihesabiki kuwa ni katika kuipokea Ramadhani, na inaunganishwa hapo swaumu zitakazokuwa za wajibu kama kulipa deni na swaumu ya nadhiri.