Muadhi alimuuliza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Kwa nini mwenye hedhi analipa swaumu na wala halipi swala?. Akasema kumwambia: Hivi wewe ni katika Makhawariji (wanaotoka katika utiifu wa kiongozi wao) wa mji wa Haruuraa wanaokithirisha maswali kwa kutaka ugumu na kutia mkazo katika dini? Akasema: Mimi si mtu kutoka Haruuraa, bali mimi ninauliza tu, akasema: Tulikuwa tukipatwa na hedhi tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi tunaamrishwa kulipa swaumu, na wala hatuamrishiwi kulipa swala.