Anaeleza Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa kipenzi chake na jamaa yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuusia na akamsisitizia mambo matatu: La kwanza: Kufunga siku tatu katika kila mwezi. La pili: Rakaa mbili za Dhuhaa kila siku. La tatu: Kusali witiri kabla ya kulala; na hii ni kwa mtu atakayehofia kutoamka mwisho wa usiku.