Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwatukana Maswahabah hasa wa mwanzo katika Muhajirina na Ansari; na akaeleza kuwa lau mmoja miongoni mwa watu angetoa dhahabu nyingi kama mlima Uhudi, zisingefikia thawabu zake kwa hilo malipo ya kibaba cha Swahaba mmoja au nusu yake - na kibaba ni kujaza viganja viwili vya mtu wa wastani-; Na hii ni kwa sababu ya ikhilas yao kuwa zaidi, na ukweli wa nia zao, na kuwahi kwao kutoa na kupigana kwao katika njia ya Mwenyezi Mungu kabla ya ufunguzi wa mji wa Makka, ambapo uhitaji wake ulikuwa mkubwa.