Kutoka kwa Katada amesema: Aliulizwa Anasi kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: "Kilikuwa ni kuvuta", kisha akasoma: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu" [Al-Faatiha:1] Alikuwa akivuta neno: Bismillaahi, na anavuta Al-Rahmaani, na anavuta neno: Al-Rahiim. Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy
explain-icon

Ufafanuzi

Aliulizwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Qur'ani? Akasema: Alikuwa akivuta sauti yake kwa kisomo; akivuta herufi Lamu ilioko kabla ya "Haa" katika neno: "Allah", na anavuta herufi "Mim" ilioko kabla ya "Nuun" katika neno "Al-Rahmaan", na anavuta herufi "Haa" katika neno "Al-Rahiim".

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kuvuta ni kuzishibisha herufi za mada nazo ni (Alif, Wau, Yaa) zinapokuwa na sakina na kabla yake kukawa haraka (silabi) inayoendana nayo.
  • Kumebainishwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Qur'ani.
  • Kutekeleza kwa vitendo kwa ajili ya kubainisha kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Amesema Assindi: Kauli yake: "Akivuta sauti yake", yaani anarefusha herufi zinazofaa kurefushwa kwa kuzitumia kuzingatia na kutafakari na kumkumbusha mwenye kukumbuka.
  • Umuhimu wa kujua kanuni za kusoma Qur'ani (Tajwidi) na elimu za Qur'ani.
  • Kuzielewa dalili kunarejeshwa kwa wanachuoni, kama alivyoulizwa Anasi radhi za Allah ziwe juu yake akambainishi muulizaji.