Alisema kiongozi wa waumini Abubakari Swiddiq radhi za Allah ziwe juu yake wakati wa kuhama: Nilitazama katika nyayo za washirikina nao wakiwa wamesimama juu ya vichwa vyetu juu ya pango na sisi tukiwa ndani yake, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau kama mmoja wao angelitazama katika nyayo zake angetuona chini ya nyayo zake, akasema: Ewe Abubakari, kwani ni ipi dhana yako kwa wawili ambao Mwenyezi Mungu ndiye wa tatu wao kwa kuwanusuru na kuwasaidia, na kuwahifadhi na kuwapa muongozo?!