Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hurejeshewa roho yake ili ajibu salam kwa kila aliyemsalimia sawa sawa awe karibu au mbali; na maisha ya Akhera na kaburini ni jambo la ghaibu, hakuna ajuaye uhalisia wake isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, naye juu ya kila kitu ni muweza.