Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kisa kinachotubainishia sisi kiwango cha mapenzi ya mswaki kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na kushikamana kwake na mswaki, na hii nikuwa Abdur Rahman bin Abiibakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kaka yake na Aisha aliingia kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa katika hali ya ulevi wa mauti. naye akiwa na mswaki mbichi, akisugua meno yake, alipouona Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki ukiwa kwa Abdur Rahman, hayakumshughulisha yale aliyonayo katika maradhi na ulevi wa kifo, kwasababu ya mapenzi yake juu ya mswaki, akanyanyua macho yake kuutazama, kama mtu mwenye shauku nao, akagundua Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akauchukua mswaki toka kwa ndugu yake, na akakipunguza kichwa cha mswaki kwa meno yake, na akausafisha na kaupendezesha, kisha akampatia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akautumia kusukutua. Aliposafishika na akamaliza kupiga mswaki, alinyanyua kidole chake -akimpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu-, na akichagua kuhamia kwa Mola wake Mtukufu, kisha akafariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-. Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akaweweseka, na ni haki yake kuwa hivyo, kwasababu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- alifariki na kichwa chake kikiwa juu ya kifua chake.