explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa hakuna waislamu wawili watakaokutana njiani na mfano wake wakasalimiana kwa kupeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana kwa viwiliwili au kwa kumaliza kupeana mikono.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Sunna ya kupeana mikono wakati wa kukutana, na himizo juu yake.
  • Amesema Manawi: Na sunna haipatikani isipokuwa kwa kuweka mkono wa kulia katika mkono wa kulia kiasi kwamba hakuna udhuru.
  • Himizo la kusambaza salamu, na kumebainishwa ukubwa wa malipo ya kumpa mkono muislamu ndugu yake muislamu.
  • Kunavuliwa katika hadithi kupeana mikono kwa haramu, kama kumpa mkono mwanamke wa kando.