Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa mkewe mama wa waumini Juwairia radhi za Allah ziwe juu yake mwanzo wa asubuhi aliposwali swala ya Alfajiri, na Juwairia akiwa kakaa mahali aliposwalia, kisha akarejea baada ya mchana kufika kati kati wakati wa dhuha, naye akiwa bado kakaa katika mahali pake, akasema: Hivi bado uko katika hali niliyokuacha nayo? Akasema: Ndio, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika nimesema baada yako maneno manne, na nimeyakiriri mara tatu, lau yangelinganishwa kulingana na malipo na yale uliyoyasema kwa muda wote uliokaa hapa basi yangeliyazidi: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" na kutakasika kwake kutokana na mapungufu, "na sifa njema ni zake" kiasi ambacho ana sifa nzuri ambazo amewaongoza kwazo, "idadi kubwa ya viumbe wake" ambazo hakuna awezaye kujua idadi yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, "na ridhaa ya nafsi yake" kwa kiasi kinachomridhisha kutoka kwa wale aliowaridhia Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake nalo ni jambo lisiloelezeka, "na uzito wa Arshi yake" ambacho ndicho kiumbe kikubwa na kizito zaidi, "na wino wa maneno yake" na maneno ya Mwenyezi Mungu hayadhibitiki kwa idadi na wala hayamaliziki; na hii inakusanya migawanyiko yote mitatu na inazienea; kwani wino wa maneno yake Mtukufu hauna mwisho wa kiwango chake, wala sifa yake, wala idadi yake, lakini makusudio yake: Ni kupita kipimo katika wingi; kwa sababu yeye ametaja mengi mwanzoni yanayoweza kuhesabika miongoni mwa viumbe, kisha akapanda juu kwa makubwa zaidi katika hayo na akayaelezea kwa neno ridhaa ya nafsi yake, kisha uzito wa kiumbe kikubwa nacho ni Arshi; vya kwanza ni vya kuhesabika na kiwango maalumu, na vya pili ni kwa sifa na namna maalumu, na vya tatu ni kwa ukubwa na uzito.