Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa njia ya kutahadharisha juu ya hatari ya ulimi, kuwa mtu mmoja aliapa kuwa Mwenyezi Mungu hatomsamehe mtu mmoja aliyekuwa akitenda madhambi; kana kwamba kamuhukumia Mwenyezi Mungu na kamfungia maamuzi; alipoamini ndani ya nafsi yake kuwa yeye kwa Mwenyezi Mungu ana ubora na thamani na nafasi, na kwa huyu mkosefu ana udhalili, na huku ni kumuelekeza Mwenyezi Mungu na ni utovu wa adabu kwake, akamuwajibishia mtu huyo tabu na hasara Duniani na Akhera.