Amemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa juu ya Mimbari yake, mwenye kuacha swala ya Ijumaa na kutohudhuria bila udhuru, kwa uvivu na uzembe, au vinginevyo Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya nyoyo zao na kuzifunika na kuziwekea kizuizi kitakachozizuia kufuata haki, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika kuzikumbuka sababu za kheri, na kinachokataa kheri ni nafsi zao wao wenyewe.