explain-icon

Ufafanuzi

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekidhi haja yake sawa iwe haja ndogo au kubwa, kustanji kwa mfupa wa mnyama au kinyesi chake na mabaki yake yaliyokauka; na akasema: Hivyo haviondoshi najisi, na wala havisafishi vizuri.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kumebainishwa baadhi ya adabu za kukidhi haja na kustanji.
  • Katazo la kustanji kwa kinyesi cha wanyama; kwa sababu: Ima ni najisi, au kwa sababu ni chakula cha wanyama wa Majini.
  • Katazo la kustanji kwa mfupa; kwa sababu ima ni najisi, au ni chakula cha Majini wenyewe.