Aliwakataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanawake kuacha mapambo kwa kuacha urembo kama marashi au wanja na mapambo mengine na nguo nzuri kwa ajili ya maiti, sawa sawa awe baba au kaka au mtoto au wengineo, zaidi ya siku tatu, isipokuwa kwa atakuwa mume ni miezi minne na siku kumi, na hatovaa katika kuacha mapambo kwa ajili ya mumewe nguo zote zelizo na urembo isipokuwa nguo yenye urembo kiasi, nayo ni nguo iliyokuwa ikitengenezwa Yemen wakati huo, hutiwa urembo kabla ya kushonwa, na wala hatopaka wanja machoni kwa ajili ya urembo wa macho, wala hatojipaka kwa harufu za marashi na nyinginezo, isipokuwa kama akioga kutokana na hedhi yake kwa kutumia kipande kidogo cha Qustwi au Adhfar, nazo ni aina mbiili maarufu za udi (anaweza kutumia udi mwingine pia) ambao lengo lake si kujipamba, umeruhusiwa kwa mwenye kuoga kutokana na hedhi, kwa ajili ya kuondoa harufu mbaya, ambayo hufuatana na athari ya damu katika tupu na si kwa ajili kujitia manukato.