Kutoka kwa Jaabir bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Kinacholewesha kikiwa kingi, basi hata kidogo ni haramu".
Ni nzuri (Hasan) - Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa kila kinywaji au chakula kinachoondosha akili wakati wa kukitumia kingi chake, basi kukitumia kidogo chake ni haramu, hata kisipoondosha akili.
Katika Faida za Hadithi
Sheria imehifadhi akili za watu.
Kufaa kuzingatia mlango wa kuzuia sababu zinazopelekea katika maovu, na hiyo ni kwa kufunga kila njia inayopelekea katika machafu hayo.
Kumeharamishwa kichache katika kilevi; kwa sababu ndio njia ya kulewa.
Kisipolewesha si kidogo wala kingi, basi hicho si haramu.