explain-icon

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumaliza swala yake anatoa salaam kuliani kwake na kushotoni kwake kwa kugeuka kwa uso wake upande wa kulia, pamoja na kusema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na anatoa salaam kushotoni kwake, kwa kugeuza uso wake upande wa kushoto, pamoja na kusema: "Assalaam alaiku warahmatullah".

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Sheria ya kutoa salaam mbili ndani ya swala, nakuwa salam hizo ni katika nguzo zake.
  • Inapendeza kuleta ziada ya kauli "wabarakaatuh", katika baadhi ya nyakati; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwa anadumu nayo.
  • Kutamka salaam mbili ndani ya swala ni nguzo ya wajibu, na ama kitendo cha kugeuka wakati wa kuzitamka ni sunna.
  • Inatakiwa iwe kauli ya: "Assalaam alaikum warahmatullaah" wakati wa kitendo cha kugeuka na si kabla yake wala baada yake.