Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyakati tatu za mchana kutoswali ndani yake swala za sunna, au kuzikwa ndani yake maiti: Wakati wa kwanza: Wakati linapodhihiri jua kwa kuchomoza, na hii ni wakati wa mwanzo wa kuchomoza kwake mpaka linyanyuke kiasi cha mkuki, na inakadiriwa kuwani robo saa takribani. Wakati wa pili: Pindi jua linapofika kati kati ya mbingu, linapokuwa halina kivuli upande wa Mashariki au Magharibi mpaka linapoondoka kutoka kati kati ya mbingu, na kikaonekena kivuli upande wa Mashariki, wakati ambapo unaanza wakati wa Adhuhuri, nao ni wakati mfupi mno; ambao ni kiasi cha dakika tano takribani. Wakati wa tatu: Linapopinda na likaanza kuzamia Magharibi mpaka lizame.