Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuingia kwa mwezi wa Ramadhani na kutoka kwake, akasema: Mtakapouona mwandamo wa Ramadhani basi fungeni, yakikukingeni mawingu kati yake na nyie, basi hesabuni siku thelathini za mwezi Shaaban, na mkiuona mwandamo wa mwezi Shawal basi fungueni, yakikukingeni mawingu na ukafichikana kwenu; basi hesabuni siku thelathini za mwezi Ramadhani.