Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako" na ninajiegemeza kwako, "Kutokana na kushindwa" kwa kukosa uwezo wa unjanja wenye manufaa, "na uvivu" kwa kushindwa kuendesha mambo, aliyeshindwa hana ujanja, na mvivu hana haja nao, "na uoga" kwa kujizuia kuyaendea yanayopasa kufanywa, "na ubahili" kwa kuzuia yanayopaswa kuyatoa, "na ukongwe" na ukubwa wa umri unaopelekea udhaifu wa mwili, "na adhabu za kaburi" na sababu zinazopelekea katika hayo. "Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu" na uipe na uiwezeshe katika "uchamungu wake" kwa kufanya uchamungu na kuacha maasi, "na uitakase" na uisafishe kutokana na uchafu na tabia mbaya, "wewe ndiye mbora wa kuitakasa" na wala hakuna wa kuitakasa yeyote zaidi yako, "Wewe ndiye msimamizi wake" na mtetezi wake na msimamizi wake, "na Mola wake" Msimamizi wa mambo yake, na Mola wake Mlezi na mwenye kuineemesha. "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyokuwa na manufaa", kama elimu ya nyota na ukuhani na uchawi, au isiyo na manufaa Akhera, au elimu isiyofanyiwa kazi, "na moyo usionyenyekea" kwako, na wala haujishushi, na wala hautulii, wala hautulizani kwa kukutaja, "na nafsi isiyoshiba" wala isiyokinai kwa yale iliyopewa na Mwenyezi Mungu na akairuzuku miongoni mwa halali nzuri, "na kutokana na maombi" yenye kurudishwa "yasiyopokelewa".