Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kuna baadhi ya watu wana nywele zilizoshikana tena zilizojaa vumbi, na hawazipaki mafuta wala hajali kuziosha, na wala hawana heshima yoyote mbele za watu, basi watu humsukuma mtu kama huyu katika milango yao, na kumfukuza kwa kumdharau; isipokuwa mtu huyu lau angeapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa litokee jambo basi Mwenyezi Mungu angelitenda jambo hilo kwa sababu ya kumkirimu na kumtukuza kwa kujibu ombi lake, na kumlinda asijekupotoka katika kiapo chake, na hii ni kwa sababu ya ubora wake na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu.