Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ibada za sunna zimekuwa nyingi kwake mpaka zikamshinda kwa sababu ya udhaifu wake, kisha akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali nyepesi itakayompa thawabu nyingi atakayoshikamana nayo na adumu nayo. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuelekeza kuwa ulimi wake uwe mbichi utikisike kwa kudumu kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kila wakati na kila hali; kama kumsabihi na kumhimidi na kumtaka msamaha na kumuomba na mfano wake.