Othman bin Abil Aswi alipata maumivu makali ambayo yalikaribia kumuua, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaenda kumtembelea, na akamfundisha dua ambayo Mwenyezi Mungu atamuondolea maradhi yaliyomfika; nayo ni aweke mkono wake juu ya mahala panapoumia, na aseme: "Bismillaah" mara tatu, kisha aseme mara saba: "Ninataka kinga" na ninajikinga na kujiweka na kujilinda (kwa Mwenyezi Mungu na kudura zake kutokana na shari za yale ninayoyapata) katika maumivu ya wakati huu (na kuyahofia) na ninahofia kutokea maumivu mengine baadaye miongoni mwa huzuni na hofu, au kuendelea kwa maradhi na yakasambaa maumivu yake katika mwili.