Anatahadharisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii na anakataza kujiombea dua mbaya na kwa watoto na mali; kwasababu dua ni jambo kubwa, anaweza kuipitisha Mwenyezi Mungu kwa waja, ikiwa itaafikiana na saa ya kujibiwa ikawa madhara yake ni kwa mwenye nayo na yale yanayomuhusu kama watoto wake na mali yake.