Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake, ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliandika ujumbe kabla ya kifo chake kwa Wafalme wa mataifa waliopembezoni mwake, akiwaita katika Uislamu; akamuandikia Kisra, nalo ni jina la kupachikwa la kila Mfalme Uajemi, na kwenda kwa Kaisari, nalo ni jina la kupachikwa kwa kila mfalme wa Roma, na kwenda kwa Najashi nalo ni jina la kupachikwa la kila mfalme wa uhabeshi. Na akaandika pia kwenda kwa kila mfalme jeuri mwenye kuwakandamiza watu, na mwenye kuwatenza nguvu, na akabainisha Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Najashi aliyetumiwa Ujumbe si Najashi yule aliyesilimu na akafariki na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamswali swala ya maiti asiyekuwepo.