Ameeleza Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa mtu atakapotoka nyumbani kwake na akasema: Bismillaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu-, Tawakkalu a'lallaahi -Nimemtegemea Mwenyezi Mungu-, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaahi- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Malaika humuita Ewe mja wa Mwenyezi Mungu umeongozwa katika njia ya haki, na umetoshelezwa mahitajio yako, na umehifadhiwa dhidi ya maadui; basi shetani aliyewakilishwa kwake hujitenga mbali naye, na hapo husema shetani mwingine kumwambia shetani huyu: utawezaje kumpoteza mtu tayari kaongozwa, na katoshelezwa, na amekingwa na mashetani wote? kwasababu yeye amesema maneno haya basi wewe hutomuweza.