explain-icon

Ufafanuzi

Katika nukuu ya maneno ya Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuna ushahidi wa uelewa wa maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wa haki za watu wa familia ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na kuwatukuza kwao na kuwaheshimu kwao, yeyote atakayekuwa ni katika watu wa familia yake na akawa kanyooka katika dini na mwenye kufuata sunna za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- basi huyo ana haki mbili: Haki ya uislamu na haki ya udugu wa karibu na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na nikuwa Abuubakari na maswahaba wengine walikuwa wakiwapenda watu wa nyumba ya Mtume na wakiusia kutendewa mazuri.

explain-icon

Ziada