Mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake akiwa tayari kajiandaa kwaajili ya safari: Ni jihadi ipi yenye thawabu nyingi? Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akamueleza kuwa jihadi bora, ni yeye kumuamrisha mema kiongozi dhalimu, au amkataze maovu, jihadi haishii pekee kupigana na makafiri, bali ina daraja, na iliyotajwa ndiyo ina malipo mengi zaidi; kwasababu inahofiwa mtu kuuawa au kukamatwa kwasababu ya ujeuri na kiburi cha kiongozi na kwasababu ya uchache wa wenye kujitosa katika hilo.