Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim
explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye alikuwa akimuandalia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake, na maji ambayo atayatumia kutawadha usiku, kisha anamuamsha Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka nyakati za usiku, wakati wowote usiku, anapoamka tu anaanza kusugua meno yake kwa mswaki; ili aondoe harufu ya mdomo ambayo hutokea mara nyingi kwasababu ya kulala, kisha anatawadha udhu wake wa swala, kisha anaswali swala za usiku.