Anatahadharisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kufanya uzembe katika swala la udhu, na kutotekeleza udhu vilivyo, na anahimiza juu ya kuzingatia kuukamilisha, na kwakuwa mwisho wa miguu mara nyingi ndio huwa hayafiki maji ya udhu, basi mapungufu yanakuwa katika twahara na swala kwasababu hiyo, na akaeleza kuwa adhabu itamiminika juu ya hilo na kwa mfanyaji wake anayefanya uzembe katika twahara yake ya kisheria.